COSTECH Yashirikiana na Wadau Muhimu Kuwajengea Uwezo Wanafunzi wa Mlengo wa Sayansi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imetoa wito kwa wanasayansi chipukizi kupitia ushiriki wa warsha iliyoendeshwa na Tume hiyo kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ikilenga kuwajengea uwezo wanafunzi wa masomo ya sayansi eneo la Bioteknolojia nchini.
Warsha hiyo imefanyika tarehe 22 Januari, 2022 katika Ukumbi wa CONAS – lecture room – Jengo la Science Complex liliopo ndani ya eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Wito huo umetolewa na mkurugenzi wa Uratibu na Uendelezaji wa Tafiti, Dkt. Zabron Bugwesa Katale kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Tume wakati akifungua Warsha ya Kuwajengea Uwezo wanafunzi wa Masomo ya Sayansi waliopo Chuo Kikuu cha Dar es salaam ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi (CONAS).

“Niwashuku sana kwasababu wengi wenu humu mmechagua masomo ya sayansi na sisi kama Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia jukumu letu mojawapo ni kuendeleza sayansi hapa chini. Ninawashukuru Taasisi ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam kwa kuwa mwenyeji wetu katika warsha hii muhimu” alisema.

Dkt. Bugwesa alishukuru na kutambua uwepo wa  mwakilishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Afisa Mazingira Mwandamizi Bw. Thomas J. Chali, Mkuu wa Idara ya ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi, Dkt. Shaaban A. Kassuwi, mwakilishi wa Shririka la Viwango Tanzania (TBS), mwakilishi kutoka Chuo Kikuu cha Kilimo Tanzania (SUA) pamoja na mwakilishi wa Kampuni ya GUAVAY inayojihusisha na utengenezaji wa mbolea asilia ya Hakika.

Aliongeza kuwa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknoljia (COSTECH) itaendelea kushirikiana na wadau wote muhimu katika kuwajengea uwezo watafiti na wanasayansi nchini ili waweze kutengenza fursa mbalimbali za kujiajiri na kuongeza tija kupitia bunifu mbalimbali zitakazoibuliwa na wanafunzi hao wa masomo ya sayansi nchini.


Pichani ni Mkurugenzi wa Uratibu na Uendelezaji wa Tafiti COSTECH, Dkt. Zabron Bugwesa Katale (Aliyesimama); Mkuu wa Idara wa Ndaki ya Sayansi Asilia na Tumizi - CONAS,  Dkt. Shaaban A. Kassuwi;  (kushoto), Mwakilishi wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Afisa Mazingira Mwandamizi Bw. Thomas J. Chali (Wa pili kushoto) na Dkt. Beatrice Shayo mara baada ya kufungua warsha wanasayansi ilyofanyika Sayansi Complex- CONAS Chuo Kikuu cha UDSM.


                                                                                                                    Picha ya pamoja ya washiriki wa Warsha