
TARATIBU ZA KUPOKEA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO
TARATIBU ZA KUPOKEA NA KUSHUGHULIKIA MALALAMIKO
COSTECH inatekeleza shughuli zake kwa kuzingatia viwango vya ubora vya ISO 9001:2015. Kwa mantiki hiyo, COSTECH imejizatiti katika kuratibu, kukuza na kuendeleza sayansi, teknolojia na ubunifu nchini kwa mujibu wa Sheria ya COSTECH ya mwaka 1986. Kwa kuwa Menejimenti ya COSTECH huhakikisha kuwa huduma zinazotolewa zinazingatia viwango vya ubora, inawajulisha wadau na wanachi kwa ujumla kwamba utaratibu unaotumika kupokea, kushughulikia na kutoa mrejsho kuhusiana na malalamiko, maoni na mapendekezo kuhusu huduma zinazotolewa na COSTECH ni kama ifuatvyo;-
Njia za Uwasilishaji
1. Sanduku la maoni ambalo lopo katika jengo la COSTECH, lililoko Kijitonyama, Dar es Salaam;
2. Wakati wa mikutano ya mara kwa mara na wadau;
3. Wakati wa vikao vya Ushauri vya Ndani vinavyoitishwa katika maeneo yaliyoathirika;
4. Wakati wa mikutano isiyo rasmi;
5. Mawasiliano ya moja kwa moja kwa kuandika barua kwa Mkurugenzi Mkuu; S.L.P. 4302, Dar Es Salaam.
6. Kupitia Barua pepe: malalamiko@costech.or.tz
7. Kwa njia ya Simu: 0754 682733
8. Kupitia mfumo wa serikali: E- mrejesho
9. Kwa kufika katika ofisi zilizoko Kijitonyama, Sayansi, Dar es Salaam
Muhimu: Malalamiko yote kuhusu unyanyasaji/uhalifu/rushwa yataelekezwa kwenye mamlaka husika si zaidi ya siku 5 baada ya kupokelewa.
Rufaa ya Malalamiko
1. Hatua ya 1: Iwapo Afisa Ushughulikiaji wa Malalamiko (GHO) hatawezi kushughulikia na kumridhisha mdau/mlalamikaji atapeleka malalamiko hayo kwenye Kamati ya Maadili ya Kutatua Migogoro na Malalamiko (GRIC).
2. Hatua ya 2: Iwapo mdau/mlalamikaji hataridhika na uamuzi uliofanywa na GRIC, malalamiko yatawasilishwa kwenye Menejimenti ya COSTECH.
3. Hatua ya 3: Iwapo mdau/mlalamikaji hajaridhika na uamuzi uliotolewa na Menejimenti ya COSTECH malalamiko yatawasilishwa kwenye Kamisheni ya COSTECH. Ikiwa malalamiko yatashughulikiwa, hakuna hatua zaidi zinazohitajika.
4. Hatua ya 4: Iwapo mdau/mlalamikaji hataridhika na uamuzi uliotolewa na Kamisheni, mdau/mlalamikaji ataweza kuendelea na kukata rufaa kwa Katibu Mkuu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
Muhimu: Katika kila hatua ya kushughulikia malalamiko, mdau/mlalamikaji atajulishwa ipasavyo.
"Sisi kwetu ni Mteja kwanza"