
COSTECH SEHEMU YA SAFARI YA MAFANIKIO SAHARA SPARKS - DKT. NUNGU
COSTECH SEHEMU YA SAFARI YA MAFANIKIO SAHARA SPARKS - DKT. NUNGU
Dar es Salaam, Jumatano, Julai 16, 2025.
Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia Tanzania (COSTECH), Dkt. Amos Nungu amesema COSTECH wamekuwa sehemu ya safari ya Sahara Sparks tangu mwanzo kabisa.
Amezungumza hayo wakati akiongea na waandishi wa habari tarehe 16 Julai, 2025 katika ofisi za Sahara Ventures kuelekea maadhimisho ya miaka 10 ya Sahara Sparks itakayofanyika tarehe 5 na 6 Septemba katika ukumbi wa Mlimani City.
Amesema waliamini katika wazo la awali – kutoa jukwaa kwa mijadala yenye athari katika ekosistemi kama wasimamizi wa sekta ya ubunifu na teknolojia nchini, waliona ni wajibu wao kuiunga mkono, hasa wakati ambapo jukwaa la aina hii halikuwepo.
Hata hivyo amesema kupitia Sahara Sparks, tumeona mabadiliko mengi katika mfumo mzima wa ubunifu, na kwa hilo, tunajivunia kuadhimisha mafanikio haya pamoja nao.