TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

COSTECH WASHIRIKIANA NA SWEDEN,SIDO KUZINDUA KITABU CHA KONGANO BUNIFU

TUME ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa ushirikiano na watu wa Swedeni na Shirika la Viwanda vidogo, SIDO wamezindua kitabu cha kongano bunifu ambacho kinalenga zaidi kuwasaidia wabunifu na watafiti katika kufanikisha zaidi bunifu na bidhaa zao sokoni.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)Dkt. Amosi Nungu amesema wamezindua kitabu ambacho kinaongelea maswala ya kongano bunifu, wakishirikiana na wenzao kutoka Swedeni na Sido.




Amesema kuandikwa kwa kitabu hiki ni sehemu ya majukumu ya COSTECH katika kuwafikia wananchi, kushirikiana nao na kutatua changamoto zilizopo kwenye jamii hasa katika maswala ya ubunifu.

Vilevile Kwenye kongano bunifu pia wanasaidia makundi ya watu mbalimbali kukutana pamoja na kutatua changamoto walizo nazo, na kitabu hiki kimeandikwa kama sehemu ya yale waliojifunza.

Ukiacha hilo amesema pia na uzoefu kwa ushirikiano wa wataalamu wa COSTECH na wenzetu kutoka Swedeni na SIDO, kwahiyo tuko na watu kutoka Vyuo Vikuu sababu ni moja ya walishiriki waliofanikiwa kupeleka wanafunzi wao katika kongano zetu kwaajili ya utafiti.

Dkt. Nungu amemalizia kwa kusema “kitabu hiki cha kongano bunifu kwa sasa kipo katika maudhui ya lugha ya kingereza kwasababu tumeshirikiana na wenzetu kutoka Swedeni, lakini baada ya uzinduzi huu maudhui ya lugha ya Kiswahili yatafuata ili ujumbe uliokusudiwa uweze kufikia watu wengi katika jamii kwa lengo la kujifunza mengi kuhusiana na kongano zetu”

Naye moja ya waandishi wa kitabu kutoka COSTECH Meneja wa upatikanaji na uendelezaji wa teknolojia Dkt. Athumani Mgumia amesema kama COSTECH tunajipongeza kufanikiwa kutengeneza muongozo, ambao unaonyesha ni jinsi gani watu wanaweza wakafanya ubunifu endelevu,

Dkt. Mgumia ameendelea kusema, moja ya lengo la COSTECH ni kusaidia wabunifu na kuratibu maswala ya ubunifu nchini, na ubunifu ufanywa na watu wengi kama watafiti kwenye vyuo vya utafiti, vyuo binafsi na wajasiliamali ambao wako tayari sokoni lakini mara nyingi bunifu zao na wengi wao hawakidhi haja ya soko la kibiashara na bunifu zao mara nyingi zinakuwa hazina tija sana, hivyo kupitia kitabu hiki tumekiandika ili tuweze kuwakutanisha watu hawa pamoja ili tuweze kujua teknolojia zinazozalishwa na watafiti ziweze kutumika na wajasiliamali kufanya bidhaa zao ziwe shindani sokoni.

“Changamoto iliopo wabunifu na watafiti sio rahisi kufanya kazi pamoja, wengine wanafanya Sayansi lakini wengine wanafanya biashara, hivyo kupitia muongozo huu tunaouzindua una miongozo zaidi ya mitano, lengo lake ni kuweka mazingira ili watafiti na wabunifu waweze kukaa pamoja wakabuni bunifu ambazo zitakua na matokeo sahihi, pia vilevile kuwezesha bunifu hizo kufika sokoni na kuweza kutumika” amesema Dkt. Mgumia.

Hata hivyo mwandishi wa kitabu hicho Dkt. Mgumia amehitimisha kwa kusema wabunifu wanapo shindana mara nyingi wanakuwa na kitu wanachokilinda ambacho ni miliki bunifu, hivyo ndio maana tumeweka muongozo ambao utaweza kutambua ni asilimia gani ya uwezo wanazozizalisha na wanawezaje kuzilinda na kuzitumia katika ushindani, aidha zaidi ya hayo kuna muongozo wa kuweza kuwasiliana na muongozo wa jinsi gani wanaweza kupeleka bidhaa zao nje ya nchi.