![](../Images/News/1738910000.jpg)
COSTECH na WFP wasaini makubaliano ya mpango kazi kuendeleza bunifu
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) na Mpango wa Chakula Duniani (WFP) wamesaini Makubaliano ya utekelezaji wa Mpango Kazi wa mwaka mmoja unaolenga kukuza teknolojia na bunifu zinazochangia maendeleo ya sekta ya kilimo, usalama wa chakula na ustawi wa jamii nchini Tanzania tarehe 21 Januari, 2025 katika ukumbi wa COSTECH.
Mkataba huu ni muendelezo wa Makubaliano yaliosainiwa baina ya COSTECH na WFP tarehe 11 Juni, 2024 kwa lengo la kuendeleza bunifu za kilimo na chakula nchini.