TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

Mwongozo wa kitaalam utakaotumika katika kuratibu na uhawilishaji teknolojia nchini


Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imesaini mkataba na kampuni ya Chuo cha Ufundi Arusha (ATC Production and Consulting Bureau PLC) kwa ajili ya kuandaa Mwongozo wa kitaalam utakaotumika katika kuratibu na uhawilishaji teknolojia nchini. 

Mwongozo huu unatarajiwa kurahisisha menejimenti ya uhawilishaji teknolojia kutoka kwa mumiliki kwenda kwa mtumiaji; utachochea kukuza bunifu ndani ya nchi;  na utasaidia katika kuimarisha ushirikiano wa kimataifa katika nyanja ya teknolojia.

Mkataba huo umesainiwa tarehe 22 Januari, 2025 katika ukumbi wa COSTECH Dar Es Salaam.