TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

COSTECH, UNDPTz na VodaComTz kushirikiana kuandaa Wiki Ya Ubunifu Tanzania 2025

Uziduzi wa ushirikiano wa kuandaa Wiki ya Ubunifu Tanzania 2025, umefanyika jijini Dar es Salaam, ambapo COSTECH, UNDP kupitia Programu ya Funguo na Vodacom Tanzania wamezindua mashirikiano hayo kwa ajili ya wiki ya ubunifu itakayofanyika Mei 12 mpaka 16, Dar es Salaam.

Wiki ya ubunifu ni jukwaa linaloleta pamoja taasisi mbalimbali, wabunifu mbalimbali katika kupeleka tasnia nzima ya ubunifu na teknolojia hapa Tanzania.

Aidha mashirikiano haya yanakwenda kujenga taifa ambalo ni endelevu, na linakuwa ni la kibunifu.

Vilevile uzinduzi wa mashirikiano haya utakuwa ni jukwaa la kuonyesha nini kinafanyika katika eneo la ubunifu na teknolojia.

Kupitia ubunifu kuna biashara nyingi zinachipuka, kuna biashara mpya, kuna teknolojia nyingi zinakuja kwa hiyo ni kwa ajili ya kutoa nafasi kwa wadau mbalimbali ambao wako katika nafasi hiyo kuonyesha wanafanya nini.

Lakini pia kusikiliza kuna mahitaji gani ya kiubunifu na kiteknolojia katika nafasi ya Tanzania ambayo inakuwa kwa kasi sana na uchumi unabadilika. 

Naye Afisa katika Mashirikiano, Promise Mwakale kutoka ukumbi mama wa bunifu wa COSTECH amesema mashirikiano walioingia yatanufaisha vijana kwa kuwa Wiki ya ubunifu itakuwa na majadiliano kwa ajili ya wanafunzi, pia itawawezesha kupata nafasi mbalimbali.

"Huu ni muda wa kukutana na wabunifu. Kama COSTECH tuna furaha kuwa sehemu ya huu ushirikiano kwa kuifanya Wiki ya Ubunifu kuwa Kubwa zaidi," amesema.