TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

COSTEH YAPOKEA UJUMBE KUTOKA SHIRIKA LA SAYANSI AFRIKA

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) imepokea ujumbe kutoka Shirika la Sayansi Africa (Science for Africa foundation) la nchini Kenya wakiambatana  na wajumbe kutoka Shirika la Viwango nchini (TBS) ili kutathmini maeneo ya ushirikiano katika sekta ya sayansi na teknolojia.

Lengo la ziara hiyo ni pamoja na kutathmini maeneo ya mashirikiano katika Sayansi na Teknolojia ikiwa ni muendelezo wa mashirikiano yaliyopo chini ya ushirikiano wa mabaraza ya utafiti kusini mwa jangwa la sahara (SGCI). 

Ziara hiyo iliofanyika Februari, 25 mwaka huu, katika ofisi za COSTECH zilizopo Jijini Dar es salaam, imekutanisha ujumbe huu pamoja na menejimenti ya COSTECH.

Aidha kupitia wasilisho la Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Bugwesa Katale ilibainika kuwa Taasisi ya Sayansi Afrika inaweza kushirikiana na COSTECH katika maeneo mahsusi ya kisera pamoja na kuhamasisha  masuala ya jinsia katika utafiti kwa mujibu wa Sera ya jinsia iliyopo COSTECH.

Pamoja na hayo, washiriki walipongeza juhudi za COSTECH katika kutekeleza programu mbalimbali zinazotokana na mashirikiano ya mabaraza ya utafiti kusini mwa jangwa la sahara.

Amesema programu hizo ni pamoja na miradi ya utafiti ambayo inalenga kuzalisha bidhaa na kupunguza utegemezi wa kuagiza bidhaa hizi nje ya nchi.