TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

COSTECH YATOA MAFUNZO YA MFUMO WA ISO 9001:2015 KWA WATUMISHI WAKE

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia  (COSTECH) imeendesha mafunzo kwa watumishi kuhusiana na mfumo wa uthibiti ubora kwa viwango vya ISO 9001:2015, kwa ajili ya kujiandaa na ukaguzi wa kwanza, baada ya kupata cheti cha ISO.

Mafunzo hayo yamefanyika Februari 25 mwaka huu,katika ofisi za COSTECH zilizopo jijini Dar Es Salaam.

Akielezea kuhusu mfumo huo, mratibu wa ISO Bi. Nichiza Malaki amesema lengo la ukaguzi ni kuangalia kama mfumo huo bado upo na  unafanya kazi, ili kusaidia kufanya maandalizi ya ukaguzi kwa kuhakikisha mahitaji yote yanazingatiwa.

Kutokana na hilo  watumishi wote wanapaswa kujiandaa vyema na kutoa ushirikiano kwa wakaguzi kutoka Shirika la Viwango Tanzania (TBS).

"Watumishi mnapaswa kijiandaa na ukaguzi huo, ikiwemo kujipanga kupitia ushirikiano pale unapohitajika,"amesema Malaki.

Mafunzo hayo yamefunguliwa na Mkurugezi wa Huduma za Taasisi Ndg. Imanuel Mgonja na kufungwa na Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Bugwesa Katale