TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

COSTECH KUANZA UJENZI WA JENGO LA STI JIJINI DODOMA

Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), imesaini mkataba na Kampuni ya TIL Construction Limited kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Jengo la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STI) Complex jijini Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Dkt. Amos Nungu amesema kuwa ujenzi huo ni sehemu ya Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.

Dkt. Nungu amesema katika mradi huo COSTECH wametengewa Sh. Bilioni 18  ambazo zitatumika kwa ajili ya kuimarisha na kuboresha menejimenti ya mifumo elimu ya juu katika kuwezesha mageuzi ya elimu kiuchumi pamoja na kuboresha miundo mbinu ya COSTECH.

“Kwa hiyo tunafanya ukarabati hapa jengo la makao makuu Dar es Salaam, tumeshapata mkandarasi, tumeshapata vibali pia tunajenga jengo Dodoma,” amesema.

Amesema kiasi hicho cha fedha Sh. Bilioni 18, jumla ya Sh. Bilioni 8 zimetengwa kwa ajili ya ujenzi wa jengo la STI - Dodoma na ukarabati wa jengo lake lililopo Dar es Salaam.

Amesema COSTECH ina imani jengo hilo litakamilika ndani ya wakati, yaani ndani ya miezi 12, na “Tutapatikana muda wowote tutakaohitajika kuhakikisha kazi haisimami,”.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TIL, Ding Fubing amesema watafanya jitihada zao zote kuhakikisha mradi huo unakamilika ndani ya muda waliopewa.