TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

MHE. KIPANGA AONGOZA UJUMBE WA TANZANIA MKUTANO WA TUME YA UMOJA WA MATAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. Omari Kipanga ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa 28 wa Tume ya Umoja wa Mataifa ya Sayansi Teknolojia kwa Maendeleo unaonfanyika Geneva Uswisi kuanzia Aprili 07 hadi 11, 2025.

Mhe. Kipanga ameambatana na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi - Zanzibar Bi. Hawaah Mbaye pamoja na watalaam na wadau wa masuala ya Sayansi Teknolojia wa nchini akiwemo Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Amos Nungu.

Katika Mkutano huo Mhe. Kipanga amewasilisha tamko juu ya matumizi ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu (STU) katika kuharakisha maendeleo na kutatua changamoto za kijamii ambapo amesisitiza juu ya manufaa ya matumizi ya tafiti na teknolojia ili kuchochea maendeleo ya nchini.