TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

PROGRAMU YA SAMIA EXTENDED SCHOLARSHIP KUTEKELEZWA KWA AWAMU TATU DKT. NUNGU

PROGRAMU YA SAMIA EXTENDED SCHOLARSHIP KUTEKELEZWA KWA AWAMU TATU DKT. NUNGU

Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH), Dkt. Amos Nungu, amesema Programu ya Samia Extended Scholarship (DS/AI+) inatekelezwa kwa hatua tatu, ambapo ya kwanza inahusisha kambi ya kitaifa ya maarifa kwa miezi kumi ili kuwapa vijana mafunzo ya uzalendo, maadili ya kitaifa na mawasiliano ya kimataifa.

Akizungumza Julai 8, 2025 jijini Arusha wakati wa uzinduzi wa programu hiyo, Dkt. Nungu alieleza kuwa hatua ya pili ni maandalizi ya kisaikolojia kwa vijana kabla ya kusoma nje ya nchi, huku hatua ya tatu ikitoa ufadhili wa masomo ya Uzamili katika Sayansi ya Data na Akili Unde kupitia ushirikiano na Taasisi ya Afrika ya  Nelson  Mandela NM-AIST
 na IIT Madras Zanzibar.

Naye, Mwenyekiti wa Kamati ya Programu hiyo, Prof. Makenya Maboko, ameishukuru Serikali kwa kuanzisha mpango huo unaowawezesha vijana wa Kitanzania kujifunza taaluma za sayansi kama data, hatua ambayo itaisaidia nchi kuendana na maendeleo ya teknolojia na kukuza uchumi.

Makamu Mkuu wa Taasisi ya NM-AIST, Prof. Maulilio Kipanyula, amesema taasisi yao imejiandaa kikamilifu kutoa mazingira bora ya mafunzo ili kuwajengea wanufaika maarifa na ujuzi wa kisasa.