COSTECH YAWASILISHA TAARIFA YA UTEKELEZAJI MRADI WA HEET
Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) ni miongoni mwa wanufaika wa Mradi wa Mageuzi ya Kiuchumi kwa Elimu ya Juu (HEET) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia ukijumuisha utekelezaji toka Vyuo Vikuu 19 na Taasisi 3 ambapo umetoa ufadhili wa fedha za mradi huo.
COSTECH ni miongoni wa Taasisi wanufaika wa mradi wa 'HEET' ukitekeleza kupitia nyanja ya kutafsiri matokeo ya utafiti kufikia hatua ya bidhaa kwa ajili ya kubiasharishwa.
Aidha, Taasisi wanufaika wa mradi kupitia Benki ya Dunia imeweka utaratibu wa kuendesha mikutano ya pamoja na wanufaika wa ufadhili huo kila baada ya miezi sita (6) ili kutathimini Maendeleo ya utekelezaji wa malengo ya mradi kwa kila Chuo na Taasisi, Benki ya Dunia inaendesha mkutano wa tatu (3) toka mradi huo uanze utekelezaji wake.
Uwasilishwaji wa Taarifa za Mradi huo yalianza tarehe 24 - 26 Oktoba 2023, ukumbi wa Ndaki ya TEHAMA (CoICT) - Jijini Dar es salaam.
COSTECH iliwasilisha Taarifa za mradi wake kupitia Mratibu Msaidizi wa mradi wa HEET, Dkt. Aloyce Minu Andrew siku ya tarehe 26 Oktoba 2023 mpaka kufikia mwezi huu Oktoba mbele ya Jumla ya Vyuo na Taasisi 22 zilizofanya mawasilisho yake pia.
Aidha alieleza matokeo makuu ya mradi ni pamoja na Vyuo Vikuu kuanzisha vituo vya kuratibu ubunifu na atamizi kwa bunifu zinazoibuliwa katika taasisi hizo. Akitolea mfano wa Chuo Kikuu cha Mbeya amesema chuo hicho kimeweza kutambua na kuatamia bunifu 21 kwa lengo la ubiasharishaji ambapo uwezo huo ni matokeo ya mafunzo yaliyoendeshwa na COSTECH katika kuvijengea uwezo vyuo vikuu hivyo wa kutambua na kuendeleza bunifu nchini.
Mradi wa HEET unatekelezwa na Vyuo Vikuu na Taasisi kwa kusimamiwa na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.