TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

“COSTECH Yasaidia Kukuza bunifu za Wanafunzi Kupitia Ruzuku ya mradi wa HEET”

Dkt. Angel Mkindi, Mratibu na Msimamizi wa Ubunifu kutoka Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, ameishukuru COSTECH kwa kutoa ruzuku, kupitia mradi wa HEET, inayowezesha kuendeleza bunifu za wanafunzi wao hadi kufikia hatua ya kibiashara.

Dkt. Mkindi alitoa shukrani hizo kwa niaba ya taasisi tano za elimu ya juu wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tatu kwa wanufaika wa ruzuku kwa bunifu zilizopita baada ya michujo.

Amesema mchakato shirikishi na mafunzo hayo yamekuwa msaada mkubwa kwa kuwasaidia kuelewa jinsi ya kusimamia uendelezaji wa bunifu vyuoni na namna ya kuandaa mpango kazi wa kila bunifu ili kurahisisha ufuatiliaji na tathimini ya viashiria matokeo, hivyo kuwa na bunifu zenye tija zitakazoweza kutatua changamoto mbalimbali za kijamii.