TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

Teknolojia ya Rafiki Briquettes imekua kivutio jijini Arusha



Serikali kupitia Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) chini ya Mfuko wa Uendelezaji wa Sayansi na Teknolojia (MTUSATE), kwa kushirikiana na Shirika la Madini la Taifa (STAMICO), imekuwa mstari wa mbele kusimamia tafiti na uzalishaji wa vyanzo mbadala vya matumizi ya nishati salama. 

Mojawapo ya miradi iliyong'ara zaidi ni Uzalishaji wa Mkaa-Mbadala wa Rafiki Briquettes unaotumika kama suluhusho la kupunguza ukataji miti na Teknolojia hiyo kuhamasisha Utunzaji wa Mazingira nchini. 

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa mstari wa mbele kuhamasisha matumizi ya nishati mbadala na ameshuhudia jitihada zinazochukuliwa kuzalisha nishati hiyo mbadala ikiwemo Mkaa wa Rafiki Briquettes.

Dkt. Samia amekuwa mtetezi na msimamizi mkubwa wa matumizi ya nishati mbadala na juhudi za makusudi za Kitaifa wa Ajenda-endelevu ya Utunzaji wa Mazingira nchini.  

Aidha, Kupitia mradi wa Kimkakati wa Rafiki Briquettes unaotekelezwa na Serikali ya Tanzania kusimamia mustakabali wa Tanzania ya Kijani na uhifadhi wa mazingira kwa ukuaji wa uchumi imara na usimamizi wa athari za mabadiliko ya Tabia Nchi. 

Bunifu ya  Rafiki Briquettes iligeuka kivutio kikubwa wakati shamrashamra za kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani     yaliofanyika tarehe 7 Machi, 2025 clock tower na kufunguliwa na Mhe. Paul C. Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Jiji hilo, Teknolojia hiyo ilikuwa suluhisho katika kuwezesha uchomaji nyama na kuwaongezea kipato wakazi wa Jiji la Arusha. 

Matumizi ya Nishati ya Rafiki Briquettes yamepokelewa vyema na  faida zake ni rafiki kwa mazingira zikidhitibi athari za uharibu wa mazingira, mabadiliko ya Tabianchi na kuunga mkono utekelezaji wa Mkakati wa Serikali ya kukuza nishati mbadala kwa utunzaji wa mazingira na maendeleo ya kijamii na kiuchumi. 

Aidha, Serikali kupitia COSTECH imendelea kufadhili Tafiti na Bunifu za kimkakati kuchochea matumizi ya  Teknolojia na bunifu ya Rafiki Briquettes kubiashariahwa katika Soko la ndani na nje ya Nchi.

Uwezeshwaji wa Shirika la Madini la STAMICO, kupitia COSTECH, umeonesha umuhimu wa uzalishaji wa nishati mbadala na rafiki kwa mazingira ikiunga mkono juhudi za Serikali ya Tanzania kutumia vyanzo-mbadala vya Sekta ya Nishati, Utafiti na kuchangia shughuli za maendeleo ya kiuchumi kwa Taasisi za umma kufanya mapokezi chanya ya Teknolojia na matumizi ya nishati hiyo mbadala na mabadiliko ya Tabia Nchi.