TANZANIA COMMISSION FOR SCIENCE AND TECHNOLOGY
(COSTECH)

News

BARAZA LA KITAIFA LA SAYANSI TEKNOLOJIA NA UBUNIFU NCHINI SIERA LEONE, LATEMBELEA COSTECH


Baraza la Kitaifa la Sayansi, Teknolojia na Ubunifu nchini Siera Leone ( NSTIC - SL) wametembelea Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa lengo la kujifunza na kuendeleza mashirikiano katika sekta inayohusiana na masuala ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.

Ziara hiyo imefanyika tarehe 17 Machi, 2025 katika ofisi za COSTECH jijini Dar Es Salaam.

Akizungumza wakati wa ziara hiyo Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH Dkt. Bugwesa Katale, amesema moja ya jukumu la COSTECH ni kuendeleza na kuimarisha ushirikiano wa kikanda na kimataifa.

"Tunafurahi kupokea wageni kutoka NSTIC - SL  lengo likiwa kubadilishana uzoefu na kuendeleza ushirikiano" amesema Dkt. Katale

Vilevile COSTECH kama mwanachama wa mabaraza ya Sayansi, Teknolojia na Ubunifu kusini mwa jangwa la Sahara, inatuongezea uwigo wa mashirikiano na kufungua fursa kwa watafiti wetu kuwa na mashirikiano na watafiti wa nje ya Tanzania, amesema Dkt. Katale 

Kwa upande wa Mratibu wa Taifa wa Baraza la Kitaifa la Sayansi Tekolojia na Ubunifu nchini Siera Leone Bi. Fatmata Kaiwa, amesema tumetembelea Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia kwa lengo la kujifunza ikiwemo  masuala yanayohusiana na muundo wa taasisi, wanavyo tekeleza sera zao na kusimamia maswala ya utafiti na ubunifu nchini Tanzania.

" Tuna mambo mengi ya kujifunza kutoka taasisi mbailimbali, na COSTECH nchini Tanzania ni Miongoni mwa taasisi inayotekeleza majukumu yake vizuri katika sekta ya Sayansi,Teknolojia na ubunifu, na vilevile inatambulika na mabaraza mengi Africa" amesema Bi. Fatmata.